Kosi la Yanga litakalowavaa Mamelodi hili hapa, Pacome, Yao, Aucho ndani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Kosi la Yanga litakalowavaa Mamelodi hili hapa, Pacome, Yao, Aucho ndani

Msafara wa kikosi cha timu ya Yanga wenye wachezaji 26 na viongozi 12 wa benchi la ufundi, unatarajiwa kusafiri leo Jumanne saa 1 asubuhi kutoka Dar es Salaam kuelekea Pretoria nchini Afrika Kusini.


Young Africans SC inakwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.


Mchezo huo utachezwa Ijumaa ya Aprili 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld uliopo Pretoria, Afrika Kusini, baada ya ule wa kwanza uliochezwa Dar es Salaam kumalizika kwa matokeo ya 0-0.


Wachezaji watakaosafiri ni; Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery, Metacha Mnata, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Yao Attohoula, Nickson Kibabage na Lomalisa Mutambala.


Wengine ni; Gift Fred, Zawadi Mauya, Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua, Kennedy Musonda, Mahlatse Makudubela, Jonas Mkude na Farid Mussa.


Pia wapo Clement Mzize, Mudathir Yahya, Khalid Aucho, Augustine Okrah, Joseph Guede, Stephane Aziz Ki, Kibwana Shomari, Denis Nkane na Salum Abubakar.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad