Huyu ndie Daktari Aliejifanyia upasuaji mwenyewe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Huyu ndie Daktari Aliejifanyia upasuaji mwenyewe


Kikundi cha wapelelezi 11 nchini Urusi walisafiri kwa takribani siku 36 kwa ajili ya kupeleleza kwenye baadhi ya mipaka nchini humo ambapo baada ya kumaliza kazi hiyo walilazimika kusalia katika bahari ya Antartic baada ya kukumbana na msimu wa theluji.


Tovuti ya Daily mail imeeleza kuwa miongoni mwa wapelelezi hao alikuwepo daktari wa upasuaji aitwaye Leonid Ivanovich Rogozov, mwenye umri wa miaka 27, ambaye wakati wa safari hiyo alikuwa akihisi maumivu makali ya tumbo.


Kwa mujibu wa dialy (shajara) ya Rogozov ilieleza kuwa anahisi kama anaugonjwa wa appendicitis’ (apendeksi) lakini aliamua kukaa kimya kutokana na kutokuwa na mtu anayeweza kumpatia msaada.


Aprili, 30, 1961 hali ilikuwa tete kwa upande wake ndipo akaona asingeweza kuvumili maumivu hayo na kuamua kuchukua maamuzi ya kujifanyia upasuaji mwenyewe.


Kutokana na maamuzi hayo aliamua kuwashirikisha wenzake na kuwaomba wamsaidie katika upasuaji huo ndipo akaamua kuchagua timu ya watu watakaomsaidia, ambapo aliwafundisha jinsi ya kuchoma sindano yenye dawa, jinsi ya kumpa hewa pindi atakapo karibia kupoteza fahamu, kushika taa, kumuwekea kioo ili aweze kuona anachokifanya.


Siku iliyofuata saa 2 asubuhi alijichoma sindano ya ganzi na baada ya dakika 15 kupita alianza kujifanyia upasuaji uliochukua takribani dakika 50 mpaka kukamilika.


Baada ya kumaliza aliwataka wasaidizi wake wamchome sindano ya usingizi na kusafisha vifaa walivyotumia katika upasuaji huo. Kwa mujibu wa wasaidizi wake waliweka wazi kuwa Rogozov alianza kurudi katika hali yake siku nne baada ya kujifanyia upasuaji huku akichukua wiki mbili tuu kurudi katika majukumu yake ya siku zote.


Timu hiyo ya wapelelezi 11 ilikaa katika bahari ya Antartic kwa mwaka mmoja na kurudi katika taifa lao Mei 29, 1962 wakiwa wazima wa afya.


Rogozov alirudi kazini katika kliniki aliyokuwa akifanya kazi na aliteuliwa kufundisha Idara ya Upasuaji Mkuu wa Taasisi ya Kwanza ya Matibabu ya Leningrad kwa maisha yake yote.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini: 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad