Apata Mshtuko Kugundua Mke Aliemuoa ni Mwanaume Mwenzake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Apata Mshtuko Kugundua Mke Aliemuoa ni Mwanaume Mwenzake


Katika hali ya kushangaza kijana mmoja wa Indonesia hivi majuzi alipata mshtuko wa maisha baada ya kugundua mwanamke aliyemuoa siku 12 nyuma, alikuwa ni mwanaume mwezake.


Mapema wiki hii, vyombo mbalimbali vya habari nchini Indonesia viliripoti mkasa huo wa kushtua ambapo mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 26 aliyetambulika kwa kifupi cha jina lake (AK) ilimlazimu kuita polisi baada ya kugundua kuwa ameoa mwanaume.


Baada ya kuhojiwa AK anasema alikutana na mwanamke huyo 'feki' kwenye mitandao ya kijamii na baada ya muda walikutana uso kwa uso.


Akiendelea kuelezea mkasa huo AK anasema, alivutiwa nae sana alipomuona kwa mara ya kwanza na kuamua kumuomba uchumba.


Inaelezwa kuwa mwanamke 'feki' aliyejitambulisha kwa jina la Adinda Kanza Azzahra muda wote wakiwa marafiki alikuwa akificha uso wake kwa hijabu, lakini AK hakuwahi kushtukia lolote.


Hatimaye wawili hao wapendanao walifunga ndoa iliyosimamiwa na kiongozi wa kidini wa Kijiji cha Wangunjaya, nyumbani kwa kina AK, huku mahari ya bibie 'feki' ikiwa ni gramu 5 za dhahabu.


Cha kushangaza hata baada ya ndoa, Adinda aliendelea kuficha uso wake mbele ya mumewe na hata kugoma kushirikiana nae kimapenzi.


Baada ya kusikia malalamiko ya mtoto wao, familia ya AK iliamua kufanya uchunguzi na ikaja kubaini ukweli kwamba mtoto wao alioa mwanaume mwenzake na ndipo wote kwa pamoja kuamua kuwashirikisha polisi.


Jamaa huyo ameshtakiwa chini ya kifungu cha 378 cha Sheria ya Jinai ya nchi hiyo na anaweza kwenda jela hadi miaka minne.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini: 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad