Simba SC kuibomoa Coastal Union, Wamtaka Hadi Kipa

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Simba SC kuibomoa Coastal Union, Wamtaka Hadi Kipa

 Simba SC kuibomoa Coastal Union, Wamtaka Hadi Kipa

Baada ya taarifa za kumpa mkataba wa awali Beki wa kati ya Coastal Union, Lameck Lawi klabu ya Simba imeendelea kuiganda timu hiyo na sasa wanafanya mpango wa kumsajili Mlinda Lango Ley Matampi raia wa Jamhuri ya Kidemkokrasi ya Congo, ambapo kama mambo yatakwenda vyema anaweza kuvaa uzi mwekundu msimu ujao.


Habari kutoka ndani ya Simba SC zinasema Matampi, ameonekana kulivutia Benchi la Ufundi la timu hiyo pamnoja na mabosi wake, hivyo kumuweka kwenye orodha ya wachezaji wanaowahitaji kama itashindikana kumbakisha Kipa wao Ayoub Lakred raia wa Morocco.


Awali klabu hiyo ilikuwa na mpango wa kumsajili Mlinda Lango kutoka Cameroon, Joseph Fabrice Ondoa ambaye anacheza soka lake nchini Ufaransa katika klabu ya Nimes Olympique inayoshiriki ligi ya National, ambayo ni Ligi Daraja la Pili nchini humo.


“Hakuna uhakika wa moja kwa moja kama Lakred anaweza kubaki au la. Hata kama anataka kubaki, lakini klabu nayo inaweza kuweka masharti ambayo tunaweza kushindwana, kwa hiyo kama ikitokea hatukuelewana, basi mbadala atakuwa ni Matampi, benchi la ufundi na uongozi umeridhishwa na kiwango chake,” kimesema chanzo chetu ndani ya klabu hiyo


Chanzo hicho kinasema tayari mazungumzo yameanza na yeye mwenyewe ameonekana kuvutiwa na ofa, huku klabu ya Simba SC ikiamini hakutokuwa na kipingamizi chochote kutoka kwenye klabu yake ya Coastal Union.


Mlinda Lango huyo ambaye aliwahi kuidakia timu ya taifa ya DR Congo, anashika nafasi ya pili nyuma ya Mlinda Lango wa Young Africans, Djigui Diarra, kukaa langoni mechi nyingi bila kuruhusu bao ‘Clean Sheets’ akiwa nazo 12, nyuma ya raia huyo wa Mali ambaye ana ‘Clean Sheet’ 13.


Coastal, ilimsajili Mlinda Lango huyo kutoka klabu ya Renaissance ya DR Congo, ambapo mbali na klabu hiyo, amezichezea klabu zote kubwa nchini humo, AS Vita, TP Mazembe, na DC Motema Pembe, pia aliwahi kucheza soka la kulipwa nchini Lebanon kwenye klabu ya Al-Ansar.


Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema ingawa wanatarajia kufanya usajili mkubwa mara tu Ligi Kuu msimu huu itakapomalizika, lakini kwa sasa siyo wakati wa kuzungumzia chochote kuhusu hilo.


“Kwa sasa bado tupo kwenye ligi, hatuzuii tetesi za usajili, lakini ukweli wa kila kitu utabainika pale ligi itakapomalizika, nani atatoka na nani ataingia Simba SC, ila ukweli kwamba tunataka kufanya usajili mkubwa,” ametamba Ahmed

_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad