Ajali Yachukua Uhai wa Watu Saba Morogoro

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Ajali Yachukua Uhai wa Watu Saba Morogoro

Watu saba wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa mkoani Morogoro baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso katika eneo la Dakawa wilayani Mvomero.Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro


Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro SACP Alex Mkama amesema tukio hilo limehusisha gari aina ya Noah yenye namba za usajili T 101 DKB iliyokuwa inatokea Dumila kwenda Morogoro mjini kugongana na lori lenye namba za usajili RS 980 ambalo lilikuwa linatokea Morogoro kwenda Dodoma.


“Tukio hilo limetokea baada ya Lori kuacha njia yake baada ya kuover take na kukutana uso kwa uso na gari ya abiria Noah na kusababisha vifo na majeruhi kama nilivyosema”amesema Kamanda wa polisi Alex Mkama


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Mvomero Dkt. Frances Mogel amesema wamepokea majeruhi saba na miili ya watu waliofariki dunia ilikuwa sita


“Leo asubuhi tulikuwa tunatokea Dumila tumepanda Noah kufika bwawa la Hatari ndio Lori likatupush uso kwa uso,tulibahatika kutoka ndio kama unavyotuona ila wenzetu wengine wamefariki akiwemo na dereva wetu,amesema Maimuna Salum manusura wa aajali

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini: 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad