Wanafunzi 194 Washika Mimba ndani ya mwezi mmoja

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

 

Wanafunzi 194 Washika Mimba ndani ya mwezi mmoja

Kwa muda wa mwezi mmoja jumla ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wapatao 194 wamebainika kupewa mimba na kukatishwa masomo yao katika wilaya ya Momba Mkoani Songwe.


Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo, wakati akizungumza na wananchi katika kijiji cha Chiwanda wilayani humo. 


Chongolo amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Momba Kenan Kihongosi, kuwatafuta na kuwachukulia hatua wale wote waliosababisha mimba hizo kwa watoto waliochini ya miaka 18 na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.


Hata hivyo ameagiza Mtendaji wa Kata ya Nkangamo na Mwenyekiti wa kijiji cha Chiwanda kutokubali kumaliza masuala hayo kienyeji, na watoe ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwani wao ndio wanawatambua wananchi katika maeneo yao.

_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad