Yanga SC Bingwa Msimu 2023- 2024

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Yanga SC Bingwa Msimu 2023- 2024

Kocha mkuu wa Yanga SC Miguel Angel Gamondi amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata alama tatu katika mchezo wa kesho jumatano ya Mei 07, 2024 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi ili kuzidi kuweka matumaini makubwa ya kushinda taji la Ligi Kuu Tanzania Bara 2023-24.



Akizungumza na waandishi wa Habari,Kocha Gamondi amesema kuwa michezo yote ya mwisho wa msimu ndani ya ligi kuu inakuwa ni  michezo migumu lakini wataingia kucheza kama mchezo wao wa fainali ili kupata ushindi ili kulisogelea taji la ligi kuu Tanzania Bara msimu  2023-24.


"Tumejipanga vizuri kupata pointi tatu katika mchezo wetu kwani sisi kila mchezo kwetu ni fainali tunaomba mashabiki wetu waje kwa wingi uwanjani tunaahidi kupata pointi tatu, amesema  Gamondi.


Kwa upande mwingine, Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar Marwa  Chamberi amesema wataingia kwa tahadhari kubwa kutokana na kuwa watakutana na timu yenye ubora wa hali ya juu msimu huu ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara.


Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi wa ligi,wanashika nafasi ya kwanza wakiwa na alama za 65  huku imebakiza alama 8 kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa ligi kuu Tanzania Bara 2023-24 huku wakiwa wamebakiza michezo 5 mpaka sasa.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad