Ndege Iliyombeba Makamu wa Rais wa Malawi Yapotea

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza HapaNdege ya Jeshi iliyokuwa imembeba Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Chilima na watu wengine tisa imetoweka.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais wa Malawi Ndege hiyo ilitoweka kwenye rada baada ya kuondoka katika mji mkuu, Lilongwe leo asubuhi (Juni 10, 2024) ambapo Ilitakiwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mzuzu, kaskazini mwa nchi hiyo, baada ya saa nne asubuhi kwa saa za Malawi

Sababu ya kutoweka kwa ndege hiyo bado haijajulikana ambapo juhudi za kuitafuta ndege hiyo zinaendelea

Chilima mwenye umri wa miaka 51 alikuwa akielekea kuiwakilisha serikali katika mazishi ya waziri wa zamani Ralph Kasambara aliyefariki dunia siku tatu zilizopita.
_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad