King Kibadeni Afunguka"Mo Dewji Aondoke tu, Wapo Wengine Wanaoweza Kuendesha Timu"

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

 

King Kibadeni Afunguka"Mo Dewji Aondoke tu, Wapo Wengine Wanaoweza Kuendesha Timu"

Mchezaji Gwiji wa Simba SC Abdallah King Kibadeni ameamua kuvunja ukimya kutokana na kile kinachoendelea katika klabu hiyo, na kumtaka MO Dewji kuachia nafasi yake ndani ya klabu hiyo.

King Kibadeni Mputa amesema kwamba Simba SC wanatakiwa kulivunja benchi lao la ufundi na kuachana na Mwekezaji wao Mohammed Dewji (MO).

“Lazima mabadiliko yapatikane sio kuivunja tu Bodi ya Wakurugenzi, bali hata wachezaji kwa sasa hivi hawako watu wanaoweza kuiendeleza ile klabu, klabu imekuwa na mambo na kiubinafsi, hawathamini watu sio mimi tu tupo wengi ambao tulipoteza ujana wetu kuitumikia Simba” Alisema Abdallah Kbadeni Maarufu kama King Kibadeni

Aidha alilizungumiza sakata la Rais wa Heshima wa Simba na Muwekezaji MO Dewji kuhusu kutaka kuondoka, amejibu kama hivi:

“MO Dewji kama anatak kuondoka si aondoke bhana, kuna watu wanapita, sasa hivi hata ukitengeneza nepi ya mtoto ukaandika Simba inauzwa, ambapo zamani ilikuwa ngumu, saivi kila kitu unakipata, hata maandazi ukiuza watanunua, sasa hivi wapo watu hata akiondoka yeye wapo watu watajitokeza, MO anatakiwa kusema tatizo liko wapi” King Kibadeni.

Benchi la ufundi la timu hiyo limemaliza msimu 2023/24 na kocha Juma Mgunda ambaye amekuwa kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo.

Kibadeni amesema kuwa Simba SC inatakiwa kufanya mabadiliko makubwa na kuongeza kuwa wao wachezaji wa zamani hawathaminiwi ndani ya kikosi hicho.

“ Inabidi wapatikane watu wengine ambao wanaweza kuipa Simba SC mafanikio ” alisema Kibadeni.

_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad