Timu Inayomtaka DENIS Nkane Hii Hapa, Mwenyewe Achoka Kukaa Benchi Yanga

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Timu Inayomtaka DENIS Nkane Hii Hapa, Mwenyewe Achoka Kukaa Benchi Yanga


WAFANYABIASHARA wa Mara wanataka kuendeleza biashara yao kwa kinda wa Yanga Denis Nkane, ilikuongeza nguvu kwenye kikosi chao ambacho kinajipanga kufuzu Ligi Kuu Tanzania Bara.

Biashara United ina hesabu kali za kushinda mechi mbili za mtoano ‘Play Off’ dhidi ya Tabora United ili kurejea Ligi Kuu na muda huohuo imekuwa kwenye hesabu za usajili.

Wakali hao kutoka Mara wanaamini msimu ujao timu yao itacheza Ligi Kuu na tayari wameanza maandalizi ambapo Winga wa Yanga, Denis Nkane ni miongoni mwa mastaa wanaowapigia hesabu.

Biashara iliyoshuka daraja mwaka 2022, inatarajia kutuma maombi Yanga ya kumpata Nkane kwa mkopo kama itapanda daraja tena.

Ikumbukwe Wanajeshi wa Mpakani hao ndio waliomtambulisha Nkane kwenye soka la ushindani baada ya kuwatumikia msimu wa 2021/22 kabla ya kutimkia Yanga hivyo wanaamini wanaweza kumpata tena staa huyo anayesugua benchi Yanga.

Denis NKANE amekuwa na msimu bora kwa upande wa timu yake, lakini yeye binafsi hakuwa na nafasi ya kupata namba kwenye jeshi Miguel Gamondi lililobeba ubingwawa 30 wa Ligi Kuu wa NBC na Kombe la Shirikisho la CRDB.

Kwa upande wake Nkane anahitaji kupata timu itakayompatia nafasi ya kucheza ili   kuendeleza kipaji chake, tofauti na sasa anavyokaa benchi anaona kipaji   chake kinakufa, huku akiwa bado ni kijana mdogo na ana ndoto kubwa za kufikambali,  ikiwezekana kucheza nje ya nchi.

_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad