Aliyekuwa Msaidizi wa IGP Sirro Apangiwa Kituo Kingine cha Kazi na Rais Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Oktoba 2017, amemuapisha Meja Jen. Issa Suleiman Nassor kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri na Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Abdulrahman Kaniki (aliyekuwa msaidizi wa IGP Sirro) kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia.

Akizungumza mara baada ya kula kiapo, Balozi Issa Suleiman Nassor amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuonyesha imani kwake na kumteua kushika nafasi hiyo na amemuahidi kuendeleza na kukuza uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Misri.

Balozi Nassor amemuahidi Mhe. Rais Magufuli kuwa atasimamia ipasavyo diplomasia ya uchumi ambayo kwa sasa ndio njia inayotumika duniani kukuza uhusiano wa kiuchumi baina ya mataifa mbalimbali.

Kwa upande wake Balozi Abdulrahman Kaniki amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumteua kushika nafasi hiyo na ameahidi kuendeleza uhusiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Zambia ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Dkt. Keneth Kaunda.

Balozi Kaniki amemuahidi Mhe. Rais Magufuli kuwa atafanyia kazi dhamira ya kuliendeleza Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) ambalo limekuwa kiungo muhimu katika nyanja ya kiuchumi kati ya nchi hizi mbili.

Hafla ya kuapishwa kwa mabalozi hao imehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Jaffar Haniu

Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

05 Oktoba, 2017



Dar es Salaam
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad