Kimenuka..Polisi Wamshikilia Mwanamke Aliyemvika Mwenzake Pete ya Uchumba Baada ya Video Kusambaa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Geita. Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mtumishi wa mgodi wa GGM, Milembe Suleiman anayetuhumiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsi moja.

Mfanyakazi huyo ambaye ni ofisa ugavi kitengo cha manunuzi anashikiliwa baada ya ‘video’ inayomwonyesha akimvisha pete ya uchumba mwanamke mwenzake kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Video hiyo ambayo imezua mijadala hasa ikizingatia kwamba iko kinyume cha utamaduni wa Kitanzania na Serikali ambayo imekuwa ikikemea na kupiga marufuku vitendo vya mapenzi ya jinsi moja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema wanamshikilia kuwa uchunguzi kwa kuwa nchi hairuhusu mambo hayo.

Ofisa Habari wa GGM, Dili Tenga amesema hayo ni masuala binafsi ya mfanyakazi hivyo wao kama mgodi hawawezi kuyazungumzia lakini wanaviachia vyombo vya dola viendelee na uchunguzi wake.

By Rehema Matowo, Mwananchi rmatowo@mwananchi.co.tz
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sina uhakika sheria inasemaje juu ya kosa la aina hii lakini nina maswali machache pamoja na maoni. Kwanza kabisa kwanini polisi waende wakamkamate mtuhumiwa mmoja peke yake?kwanini huyo mwanamke mwengine asikamatwe? Kuonesha kuwa serikali na mamlaka husika kukerwa na jambo hilo na kuwa fundisho kwa wengine kutotenda tendo hilo tena kwanini wahusika wote katika sherehe hiyo wasikamatwe? Kuna wale walioitanagaza sherehe hiyo mitandaoni kwanini wasikamatwe? Kuna wale waliohudhuria ile sherehe kwani wote ni wacenge kwanini wasikamatwe? Huwezi kuhudhuria na kusherekea harusi ya wacenge kama wewe mwenyewe si miongoni mwao. Tunaomba vyombo vya dola vitende haki kulingana na ukubwa wa tatizo na haki.

    ReplyDelete

Top Post Ad