Rais Kikwete Amtaja Mhusika wa Sakata la Richmond....Asema ni Yule Anayetembea na Tundu Lissu Kila Siku Kwenye Kampeni

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Rais Jakaya Kikwete amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani.

Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond.

“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Kikwete.

Kabla ya mkutano huo, Rais Kikwete alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo limejengwa kwa Sh7 bilioni.

Akifungua jengo hilo, aliwaomba wawekezaji na mifuko ya kijamii kuiga mfano wa NSSF kwa kuwekeza katika sekta ya majengo kwa kuwa yanapendezesha mji.

Kadhalika, Rais Kikwete alizindua jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na nyumba 36 za bei nafuu zilizopo katika eneo la Mlole, Kigoma Mjini.

Suala la Richmond imekuwa moja ya ajenda za CCM katika kampeni za urais hasa baada ya Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyejiuzulu wadhifa huyo kwa kashfa hiyo kuhamia upinzani.

Kila sehemu ambako mgombea urais wa CCM anakwenda, suala hilo limekuwa likiibuliwa, huku Lowassa akisema yeye hakuhusika, bali alijiuzulu kuiokoa Serikali isianguke kwa kuwa ulikuwa uamuzi wa wakubwa.

Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amekuwa akienda mbali zaidi akisema akichaguliwa ataanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi wanaosababisha umaskini nchini.
_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Uyo ndio Raisi wetu Kikwete tunakupendaje

    ReplyDelete
  2. Hapo picha ndio inaanza,
    Sema Babaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  3. Ngoma nzito haya sasa UKAWA mlichokua mkikitafuta mtakipata Lisu umepewa nafasi uanze kumwaga kisamvu yeye Kikwete atamalizia kumwaga ugali tuone nani dume

    ReplyDelete
  4. Haha haha haha haha uwiiiiiiiiiiiiiiiiii hahahaha muheshimiwa raid kikwete u make funny hahahahahaha kama ulijua lowassa mwizi na alikuwa mfanyakazi wako ulie mteua mwenyewe kwanini kama raid hukumuajibisha kweli rais sasa unahitaji kupumzika tu baba man's siku sinyingi zitakuruka haha haha haha haha unatia aibu kiukweli

    ReplyDelete
  5. WOTE NI WALE WALE, WAMEHUJUMU NCHI NA KULETA UMASKINI TANZANIA.. WASIJITETEEE

    ReplyDelete
  6. Unampendaje kwa kukuongezea umaskini?au wewe fisadi?

    ReplyDelete
  7. Kama ndiye kwanini usimshitaki? Ili serikali ijisafishe. Vingnevyo watu bado tutaamini siasa za usanii

    ReplyDelete
  8. Ni vema ukamfungulia mashitata kama ni kweli, vngnevyo ni siasa za kutupiana mpira ambazo tumezichoka

    ReplyDelete
  9. Mbona hukumpeleka mahakamani n.a. kumchukulia dheria. No aibu kwa raisi kujibishana kimaneno wakati sheria unto mdomoni. Miaka 8 umekaa kimya. Kinachokufanya Leo ukixungumze ni nini.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kamjibu Tundu Lisu alomuuliza.....upo?

      Delete
  10. Ni wewe Mzee umetunza hayo, umejinadi na kujinufaisha, hujampeleka hata mmoja kortini kwani wote watakugeuzia kibao.

    ReplyDelete

Top Post Ad