Achomwa kisu na kufariki dunia akielekea kuoga kisa wivu wa mapenzi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza  ACP. Muliro Jumanne Muliro amesema kuwa katika tukio la kwanza katika kitongoji cha Bukelebe kijiji cha Kanyama kata ya Bujora Wilaya ya Magu mkoani humo alikamatwa Bw.Tubeti Matiko (24) mkazi wa Kijiji cha Kanyama Kabila ni Mkurya anayejishughulisha na ufundi Ujenzi kwa tuhuma za kumuua kwa kuchoma  na kisu kifuani na kusababisha kifo Bw.Mahige Chacha(24) Mkurya ambaye pia ni fundi ujenzi na  mkazi wa kijiji cha Kanyama mkoani humo. 

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa aliyekeleza mauaji hayo baada ya kumvizia marehemu akiwa anaelekea mtoni kuoga ambapo imeelezwa kiwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa Mapenzi kwani inadaiwa kuwa vijana hao walikuwa wakimgombania msichana ambaye jina lake limehifadhiwa ila ni mkazi wa kitongoji cha Bukelebe na upelelezi wa shauri hili ukikamilishwa na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani,Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Sekou Toure kwa uchunguzi zaidi wa madktari na ukikamilika utahifadhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi. 

Katika tukio la pili mnamo Juni 20,2020 katika barabara ya Pamba yenye msongamano wa watu wengi gari namba T.312 DFA  aina ya Mitsubish Fuso iliyokuwa ikiendeshwa na dereva anayefahamika kwa jina la Lameck Mmari (48) Mchaga mkazi wa Buhongwa akitokea eneo la Sahara kuelekea Makutano ya barabara ya Picha ya Mwl.Nyerere katika ya mji wa Mwanza aliwagonga wafanyabiashara waliokuwa wamepanga biashara zao karibu na barabara pamoja na watembea kwa miguu na kusababisha vifo kwa watu wawili ambao ni Mayala (23) Msukuma ambaye ni mfanyabiashara wa Nanasi na Mkazi wa Malimbe,Mwingine aliyefariki ni Sophia Masatu (38) Muha na mkazi wa Mbugani,ambapo wawili hao walifariki wakati wakiendelea kupatiwa matibabu. 

Kamanda Muliro amesema kuwa katika ajali wamejeruhiwa pia watu sita ambao ni Rosemary Wambura(42) Mngulimi na mkazi wa Muleba,Teddy Sayi (28)Msukuma mkazi wa Mji Mwema,Christina Sylivester(16)  Muiraq Ambaye ni mwanafunzi kidato cha tatu katika shule ya sekondari Igoma,Felister Mabula (16) Msukuma Mkazi wa mji wa mji Mwema,Joseph Daniel (29)Mjita mkazi wa Buswelu na Eric Richard(24) Mfanyabiashara wa viatu Mkazi wa Mbugani. 

Aidha kati ya majeruhi hao watatu wameruhusiwa baada ya hali zao kuendelea vizuri huku wengine wakiendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa ya Bugando huku hali zao zikiendelea kuimarika. 
Miili ya Marehemu imehifadhiwa hospitalini hapo kwa uchunguzi wa madaktari. 

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linamshikilia dereva wa gari hilo kwa ajili ya  mahojiano na uchunguzi wa awali unaonesha uwepo wa hitilafu za breki katia gari hilo na uzembe ila uchunguzi wa kina unaendelea. 

Hata hivyo Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linaendelea kuwataka madereva kufuata sheria na alama za usalama barabarani na kuheshimu watumiaji wengine wa barabara,pia linatoa rai kwa jamii hususan vijana kutafuta njia sahihi ya kutatua migogoro yao hasa ya kimapenzi ili kujiepusha na matukio ya kijinai yasiyo ya lazima yanayopelekea kujikuta wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola. 


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad