8/06/2020

Afrika Kusini ndio taifa lililoathirika kwa kiasi kikubwa na maambukizi ya covid-19Idadi ya watu ambao wamekwishaambukiwa virusi vya corona ulimwenguni, idadi yake imefikia watu  milioni  18,7 huku  idadi ya watu waliofariki ikiripotiwa kufikia watu   704 632. 


Idadi ya jumla ya watu ambao wamekwishapona vilevile baada ya kupatiwa matibabu  inaendelea kuongezeka, idadi hiyo imefahamishwa kufikia watu   zaidi ya   milioni 11,9 kote ulimwenguni. 


Ndani ya masaa 24  nchini India , watu  904 wamefariki kwa maambukizi ya virusi vya corona. 

Vifo hivyo  ambavyo vimetokea ndani ya masaa 24 vimepelekea idadi ya watu ambao wamekwishafariki kutomana na maambukizi ya virusi hivyo kufikia watu  40 772. 


Idadi ya watu ambao wamekwishaambukiwa covid-19 nchini India inaripotiwa kufikia watu   milioni  1,9. 


Katika jimbo la Gujarat,  ajali ya moto iliotokea katika hospitali moja imepelekea vifo vya watu  wanane. 


Nchini Urusi,  watu  14 606 wamekwishafariki huku watu  871 894 wakiwa na maambukizi. 

Nchini Iran ni watu  17 802 ndio ambao wamekwishafariki kwa virusi hivyo huku idadi ya watu walşoathirika na maambukizi ya covid-19 ikiripotiwa kuwa watu  317 483. 


Nchini Pakistani, watu   6035 wamefariki, nchini Indoneaia watu  5 452 wamefariki, nchini Irak watu  5 094 na nchini Saudia ni watu  3020 ndşo ambao wameripotiwa kufariki. 


Idadi ya watu ambao wamekwishafariki kwa covid-19 barani Afrika imefikia watu  21 679. 


Idadi kubwa ya watu waliofariki kwa covid-19 barani humo inapatikana nchini Afrika Kusini ambapo watu  9298 wamefariki. 


Nchini Misri ni wa  4930 na nchini Algeria ni watu  1261 ndio waliofariki  kwa maambukizi  hayo.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Featured post

Tovuti bora zaidi ya utabiri wa Soka Tanzania inakutuza shati ya Alex Iwobi iliyotiwa sahihi.

Jiunge nasi ili uweze kuweka dau kama mtaalamu na kubeti Ligi ya England, La Liga, ikiwemo jackpot. Tunakupa habari za mpira wa miguu na ...

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger