Namna Biashara ya 'Network Marketing' ilivyonipeleka Polisi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mwaka wa kimasomo 2013/2014 niliingia UDSM nikiwa na Moto wa kusoma huku nimekosa Mkopo 100% (sikupata hata baada ya ku-appeal Mara 2). Moja ya mipango yangu ilikuwa ni kufanya Mishe ya kuniingizia kipato.

Baada ya kusoma kitabu Cha Bwana Emilian Busara na Mrembo Grace kuhusu HISA, AKIBA NA UWEKEZAJI nilianza kuwekeza katika Solo la hisa la Dar es Salaam (DSE) nikitumia Pocket money yangu. Hisa za CRDB, TBL, Maendeleo Bank, na hata Swissport nilikuwa nacheza nazo Sana.

Baada ya muda kupita, Ilizuka biashara moja ambayo binafsi sikuielewa kwa Wakati huo. Ila Classmates wenzangu wachache walionekana kuvutiwa nayo Sana na kuiongelea mno. Nilipoelekezwa Mara ya kwanza sikuielewa kabisa labda kwasababu sikuwahi kuona biashara ikifanyika nanna ile.

Baadaye nilikuja kuielewa baada ya kutumiwa video presentation ya jamaa mmoja ambaye aliianza akiwa chuo Tena UD palepale na muda huo akiwa anarekodi hiyo video alikuwa anaenjoy Sana maisha. Anasafiri Sana duniani, anamiliki Discovery moja Matata, mkwanja wake kwa mwezi ni HATARI

That day niliona Kama vile MUNGU kanishushia Neema ambayo nilikuwa naihitaji muda mrefu Sana. Nilianza kufikiria namna nitakavyoboresha maisha ya familia yangu, pamoja na Mimi mwenyewe. Nilianza kuona namiliki gari kabla sijamaliza chuo, nikisafiri dunia, nikitambulika, nk

To cut the story short, baada ya muda nilijiunga kwa kusaidiwa na aliyenionyesha biashara na nikawa 'New FBO'. Baada ya ku-Hustle Sana nikaja nikapanda cheo (level) ambayo 'kwenye Makaratasi' natakiwa niwe naingiza kuanzia 500k Hadi 800k ingawa kwa ground Mambo hayakuwa hivyo.

So Wakati napanda hicho cheo nilipaswa kukamilisha points (mauzo ya bidhaa) Mimi pamoja na timu. Pale tulikuwa tunawekewa Mindset ya ku-push KWA KILA NAMNA Hadi kieleweke na kutokata tamaa. So ikabidi nianze kupiga simu kukopa hela that night. Deadline ilikuwa ni saa 6 usiku.

Baada ya muda nilimpigia jamaa ambaye Sijawahi kumuona Wala kukutana naye Ila alikuwa anafanya hiyo biashara mkoani. Tulionana kwenye group la WhatsApp la timu yetu (wote tulio chini ya Aliyetuonyesha biashara). Nikambembeleza jamaa Hadi akanipa 400k kudadeki. So nikamalizia

Hesabu zangu ni kuwa kuanzia mwezi ujao ningelipwa kuanzia 500k Hadi 800k so ningemrudishia Mwana hela yake na ningeendelea na Mishe zangu.

Hapa ndipo Mambo yalipoanzia kwenda kushoto. Mwezi uliofuatia hakuna mkwanja ulioingia KABISA. Hata Tsh 10 sikukuta.

Kufuatilia nikaambiwa kuwa Kuna tatizo lilitokea Wkt najiunga so Wakati nadhani nilikuwa eligible kupata huo mkwanja, kumbe I wasn't.
Nguvu ziliniishia hii siku. Mbaya zaidi ni kuwa huku kitaa watu wananipongeza na kuona Kama vile nimeshatoka kimaisha Wakati Mambo ni tofauti

Baada ya miezi 2 ya kumzungusha jamaa, alikuja kunifanyia Mishe moja Matata.

Kumbe jamaa alikuja Dar kimya kimya (Kutoka Mtwara anapoishi) akamtafuta dada yake (mwalimu shule Fulani Sinza) akampa namba zangu anitafute Kama vile anahitaji bidhaa ninazouza.

Baada ya kupokea simu nilifurahi na nikamuibukia kule shule bila kujua kuwa najipeleka kwenye tundu la Simba. Na hata nilipofika sikuweza kumtambua mshikaji kwasababu hatukuwahi kuonana Mimi nikadhani ni mwalimu mwenzake Kumbe jamaa ananichora tu ninavyoelezea bidhaa.

Mwishoni akaniuliza unamfahamu mtu anaitwa ___? (Jina la mwana) nikamjibu Ndiyo. Akaniuliza unamfahamu vipi? Nikamjibu pia kuwa tupo naye timu moja katika biashara Ila sikumwambia ishu za kumkopa mwana. Basi akaniambia "huyo uliyekaa naye hapo ndio huyo jamaa Mimi ni dada yake"

Hapa ndipo nilihisi miguu kuishiwa nguvu, jasho la ulimi likinitoka, na hata haja kubwa na ndogo zilianza kuja bila utaratibu waungwana. Acheni kabisa haya Mambo. Nilijiona mjinga Sana hii siku na nikajua kuwa kweli 'Za mwizi ni Arobaini'

Maswali yaliyofuata baada ya hapo sikuweza kuyajibu kiufasaha Tena. Ile confidence ya kuelezea 'ALOEVERA' ilipotea kabisa.
Mbaya zaidi kila nikiwaelezea situation ilivyokuwa hawakunielewa na mwisho wakaamua kuniitia polisi wakisema Mimi ni TAPELI . I wanted to cry that day.

Nilijaribu kupiga simu kwa viongozi wangu japo wanikope hata 200k ya kumfukuza mwana lakini wote waliniambia WAMEFULIA. Hapa ndipo nilipojua kuwa nipo Kwenye BIASHARA ISIYONIFAA. Yaani mtu anayetuambia anaingiza 3-6 Million na yeye Hana hata Senti au hawezi kunisaidia?

So mwisho nilipelekwa kituo Cha Polisi SHEKILANGO pale. Yule mwalimu (dada wa jamaa) alikuwa anafahamiana na afande mmoja. That was a first day napelekwa kituoni Tena nikiitwa TAPELI na MWIZI. it was embarrassing.

Hizi biashara Sio...

Ni Mungu tu aisee aliyefanya nitoke Polisi that day. Niliweka Bondi devices zangu pamoja na zile bidhaa zote ndipo tukaandikishiana pale mbele ya afande.Hivyo ndivyo nilivyotoka siku ile. Hela zote mfukoni walibeba bahati nzuri nilikuwa na hela ndogo kwenye soksi ndio ikawa nauli

Toka siku hiyo, sikutaka kusikia Tena ishu za ile biashara. I started to be dormant and baada ya muda niliiacha. Kuna sababu nyingine nyingi pia zilichangia Ila Leo tuijue hiyo moja tu.

Mpaka Leo sitaki kuzisikia hizo kampuni zinazoendesha hizo biashara. KABISA.

---MWISHO-

Mwana.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad