8/14/2020

Ofisi za CHADEMA zachomwa, waeleza kilichojiri


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa CHADEMA Tumaini Makene amesema kuwa tukio la ofisi za chama hicho Kanda ya Kaskazini kuchomwa moto na wasiojulikana si jambo jema ukizingatia leo Mgombea Urais wa chama hicho Tundu Lissu atakuwa Arusha.


Makene ametoa kauli hiyo hii leo Agosti 14, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, na kuongeza kuwa na hata mlinzi wa ofisi hizo mpaka sasa hivi hajulikani alipo na hata simu zake hazipatikani.

"Taarifa za awali usiku wa kuamkia leo watu wasiojulikana wamevamia na kumwagia Petroli jengo la Ofisi za Kanda ya Kaskazini,  na bahati mbaya hata mlinzi wa ofisi hizo hajulikani yuko wapi baada ya tukio hilo, ni tukio baya kwa sababu hata mgombea wetu wa Urais anaingia Jiji la Arusha leo" amesema Makene.

Ofisi za chama hicho Kanda ya Kaskazini zimeungua moto usiku wa kuamkia leo, baada ya watu wasiojulikana kumwagia Petroli jengo hilo na kisha kulilipua.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

2 comments:

 1. What a Dramatic Scene..!!!

  The only one to expllain its planning and execution is not other than Godiless Faru Joni and Mlinzi.
  ukizingatia kuanzia J4 baadhi ya vitu vilianza kutolewa kwa ajili ya maatayarisho ya tukio for Media propaganda. Mmekula kwenu.

  ReplyDelete
 2. What a perfect Dramatic Scene..!!!

  The only one to explain, its planning stage and its execution is non other than Godiless Faru Joni and Mlinzi.
  ukizingatia kuanzia J4 baadhi ya vitu vilianza kutolewa kwa ajili ya maatayarisho ya tukio for Media propaganda. Imekula kwenu.

  ReplyDelete

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger