8/11/2020

Tetesi za Usajili: Yanga kumshusha Patrick Aussems ‘Uchebe’ , Simba Kumchukua Papy Kabamba TshimbiMara baada ya Mnyama Simba kumsajili na kumtambulisha rasmi, Bernard Morrison akitokea Yanga nikama vile Wananchi wamechokozwa maana baada ya masaa 24 tu kupita ghafla Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Senzo Mazingisa akatangaza kujiuzulu.
Lakini kama hiyo haitoshi hazikupita hata dakika zikazuka taarifa kuwa mtu huyo aliyekuwa muhimu ndani ya Simba na kama angekuwa mchezaji basi angekuwa kiungo mchezeshaji kwa namna alivyo bobea na kuwa muhimu pale Kariakoo lakini ikaonekana picha akisaini katika timu ya Wananchi licha ya kuwa mpaka sasa upande wa Jangwani umekaa kimya bila kuongea chochote.
Tetesi zilizopo kwa hivi sasa Yanga wanamrejesha aliyekuwa kocha wa Simba, Patrick Aussems ‘Uchebe’ huku wakitishia tishia kumng’oa Clatous Chama.


Katika tetesi zilizopo ambazo zinazungumzwa kwenye dirisha hili la usajili ni pamoja na Deo Kanda inadaiwa huwenda akatangazwa kwa Wananchi na kilichopo ni swala la muda.


Papy Kabamba Tshimbi inadaiwa anaelekea kwa Mabingwa wa Nchi, Mnyama Simba.


Hizi ni tetesi tu, katika dirisha hili la usajili linaloendelea hapa nchini, ukweli wa yote utajulika tu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger