MKE WA MUGABE AITWA MAHAKAMANI KWA KUMZIKA MUMEWE KINYUME NA MILA ZA ZVIMBA

 


Mahakama ya Kimila Nchini Zimbabwe imemtaka Grace Mugabe kufika Mahakamani hapo kwa tuhuma za kufanya mazishi yasiyofaa kwa Hayati Rais Robert Mugabe


Grace Mugabe anatuhumiwa kwenda kinyume na Utamaduni wa Jamii yao kwa kumzika Mume wake katika Boma la Familia badala ya kumzika sehemu iliyochaguliwa na Jamaa zake


Waraka kutoka kwa Chifu Zvimba umesema Grace anatakiwa kuufukua mwili wa Hayati Mugabe ili uzikwe tena kulingana na utamaduni wa Watu wa Zvimba. Pia, ameagizwa kulipa faini ya Ng’ombe na Mbuzi kwa kukiuka utamaduni


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE