.

8/17/2021

Msemaji wa Simba Kamwaga Akanusha Tetesi za Kubwaga Manyanga Simba
Uongo wa kupuuzwa

Nimeshangazwa na taarifa hizi zinazosambazwa na waandishi wenzangu - wengine wazoefu, kuhusu mimi kubwaga manyanga Simba.

Wengine wamenipigia simu ku 'balance' wakati tayari wameshasababisha taharuki isiyo na sababu kwa viongozi wangu, wanachama wenzangu na washabiki wa Simba kwa ujumla.

Nimepewa majukumu yangu mahususi Simba kwa muda wa miezi miwili na bado kazi hiyo sijaikamilisha. Nimedhamiria kukamilisha majukumu hayo mpaka ukomo wake.

Baada ya kuona usajili wa aina yake na mipango mikubwa mikubwa ya Simba ikiwa inatekelezwa, wabaya wetu wameibuka na uongo mwingine. Njia ya mwongo ni fupi.

Mimi bado nipo Simba. Tena bado nipo sana. Uongo huu dhidi yangu na Simba SC upuuzwe.

Ezekiel Kamwaga
Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano

Simba SC

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger