Ticker

6/recent/ticker-posts

Jezi za Yanga zampagawisha Jokate… ampa neno Vunjabei

MKUU wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo amesema licha ya kwamba jezi za Simba ni nzuri ila za Yanga ni kiboko. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam… (endelea). 

Aidha, Mwegelo amempongeza mfanyabiashara Fred Ngajiro ‘Vunjabei’ ambaye ana zabuni ya kutengeneza na kusambaza jezi Simba kwa kazi nzuri aliyoifanya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mwegelo amesema kati ya vitu vinavyotoa hamasa kwa vijana ni pale kijana anapoaminiwa na kufanya vyema.

“Leo nimeona nikampongeze @fred_vunjabei kwa kazi nzuri aliyoifanya na kutupa heshima kubwa vijana wa Kitanzania kwamba tunaweza.

“Rai yangu kwa vijana wote ukiaminiwa onesha uwezo .Kweli uzi ni mkali Ila wa Jangwani kiboko yao,’ ameandika Mwegelo kisha Vunjabei akajibu;

“Asante rafiki angu mkyuti, Simu yangu ni moja tu siku ya Simba day tunaomba ulinzi.”

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments