Baada ya Kuonyeshwa Video Tatu tu Kocha Simba Akubali Chama Atue Simba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





VIDEO tatu ambazo amepewa Kocha Mkuu wa mpya wa Simba Mhispania, Franco Pablo zimetosha kumshawishi kumrejesha kiungo mshambuliaji fundi Mzambia Clatous Chama.


Hiyo ikiwa ni siku chache tangu kocha huyo apewe jina la kiungo huyo ambaye inadaiwa ameomba kurejea katika timu hiyo baada ya kukosa furaha katika klabu yake mpya ya RS Berkane ya nchini Morocco.

Chama alijiunga na Berkane katika msimu huu baada ya Simba kumuuza kwa dau la Sh 1Bil akisaini mkataba wa miaka miwili.


Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya Benchi la Ufundi la timu hiyo, kocha huyo aliomba kutazama video hizo za michezo iliyopita akiwa Simba kwa lengo la kujiridhisha uwezo wake.



Chanzo hicho kilisema kuwa video zilitosha kumshawishi Pablo na kuomba kiungo asajiliwe haraka kama uongozi
utakuwa na mkwanja wa kutosha kuvunja mkataba Berkane.


Kiliongeza kuwa kocha huyo alisema kwa kiwango ambacho kiungo huyo kinatosha kabisa kuingia moja kwa moja katika mfumo uchezaji.


“Kocha Pablo alisikia tetesi za kiungo huyo kutajwa kurejeshwa katika timu, hivyo aliomba video za michezo mitatu ambayo Chama amecheza akiwa na Simba.



“Kikubwa alitaka kujiridhisha kwa ajili ya kuangalia uwezo wake na kama ataweza kuingia katika mfumo wake na aina ya uchezaji wa soka la pasi hasa 68 ikiwa na mpira.


“Baada ya kuziangalia video hizo kocha akapendekeza kurejeshwa kwa Chama kama watakuwa na fedha za
kuvunja mkataba wake huko anapocheza,” alisema mtoa taarifa huyo.


Akizungumzia hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema kuwa:
“Chama hapa ni nyumbani muda wowote atarejea, kwani hakuondoka kwa ubaya na sisi ndiyo tulimuuza.

Kikubwa usajili wetu tunaufanya kwa kupitia mapendekezo ya kocha wetu, hivyo kama akimuhitaji basi tutamrejesha kikosini.”

Stori na Wilbert Molandi na Musa Mateja

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad