3/07/2022

Ghala la Mafuta Ukraine Lapigwa Kombora na Urusi

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza >> HAPA


Moto mkubwa umezuka katika ghala kubwa la mafuta katika Mji wa Luhansk, Ukraine asubuhi ya leo baada ya ghala hilo kupigwa na makombora na kusababisha mlipuko mkubwa.

Kwa mujibu wa mashuhuda, kabla moto mkubwa haujaanza kuwaka, kilisikika kishindo kikubwa ambacho bila hata kuuliza kila aliyekisikia alijua kuwa ni cha makombora.

Muda mfupi baada ya kishindo hicho, ndipo mlipuko mkubwa ulipotokea na kusababisha moshi mzito na moto mkubwa kutanda eneo hilo.

Mshauri wa Kiongozi wa Chama cha LPR (Luhansk People's Republic) kinachowania kujitenga katika jimbo hilo, Rodion Miroshnik, amelituhumu Jeshi la Ukraine kwamba ndiyo lililofanya shambulio hilo na si majeshi ya Urusi kama wengi wanavyoweza kudhani.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger