4/15/2022

Familia ya Ricketts Imesitisha Ofa Yao ya Kuinunua Klabu ya Chelsea

TAARIFA iliyotolewa na Kampuni ya uwekezaji ya Ricketts imedai kuwa wameamua kujitoa kutokana na mambo kadhaa kutoelezewa vizuri juu ya mustakabali wa uwekezaji wao ndani ya klabu ya Chelsea.

 

Wawekezaji hao wamekuwa wakipingwa vikali na mashabiki wa Chelsea kutokana na kuwa na tuhuma za ubaguzi.

 

Kabla ya kujiondoa katika mbio za kuinunua klabu hiyo yenye maskani yake jijini London familia ya Ricketts iliungana na muwekezaji mwenza Ken Griffin ili kufanikisha ununuzi wa klabu hiyo.Japo wachambuzi wa masuala ya michezo wanasema changamoto yta kujitoa kwa familia ya Ricketts ni kutokana na kutokuwepo makubaliano ya mgawanyo wa hisa baina yao.

 

Katika taarifa yao wameelezea mapenzi yao kwa klabu na kumtakia kila lakheri muwekezaji mpya atakayeichukua klabu ya Chelsea

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger