Ahmed Ally arudisha majibu Young Africans "Mkitaka Tunawapa Morison Kwa Mkopo"

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amejibu sakata la Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison kuhusishwa na kurudi Young Africans, baada ya mkataba wake kufikia kikomo Msimbazi mwishoni mwa msimu huu.

Tangu mwanzoni mwa juma hili, taarifa zinasema kuwa, Morrison amedhamiria kurudi Young Africans baada ya kuzungumza na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo, ambao wanataka kuona akirudi kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.

Ahmed Ally alizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo wa jana Jumatano (Mei 11) dhidi ya Kagera Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Ahmed amesema taarifa za Morrison kuhusishwa na upande wa Young Africans amezisikia, lakini anaamini hata kama mchezaji huyo atakwenda huko, haitawezekana kwa wahusika kufika hatua ya Robo Fainali Kimataifa.

“Kwani wanafikiri wakimchukua Morrison atawafikisha Robo Fainali? Tukitaka tunaweza kuwapa kwa mkopo Morrison au mchezaji yoyote halafu tuone watafika wapi.” amesema Ahmed Ally

Morrison alisajiliwa Simba SC mwanzoni mwa msimu uliopita, baada ya kumaliza mkataba wake na Young Africans licha ya kuibuka kwa sintofahamu kati yake na viongozi wa klabu hiyo ambayo ilimleta nchini wakati wa Dirisha Dogo la Usajili msimu wa 2019/2020.

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad