Ticker

6/recent/ticker-posts

Panya Road Afunguka Jinsi Wanavyofanya Uhalifu "Tunaiba Alafu Tunagawana"

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema limeendelea kuisimamia operesheni maalum kali na msako wa mtaa kwa mtaa dhidi ya Vijana wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu maarufu Panya Road na mpaka May 6,2022  limewakamata Wahalifu 31 kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya uporaji baada ya kuvunja nyumba, kujeruhi na kuiba vitu mbalimbali vya nyumbani.

Miongoni mwa waliokamatwa ni Yunus Jafar Kwalo (20) ambaye amesimulia jinsi wanavyofanya uhalifu.

"Matukio yetu ya kiuhalifu huwa tunafanya usiku, tunakutania Mtaa wa Msumbiji (Chanika) Mnara wa Voda, suala la kuiba huwa halipangwi Watu wanatoka na kuingia kila nyumba baada ya hapo kuna Mtu anachukua vile vitu na kuondoka navyo na kisha vinauzwa mnagawana hela"

"Anayetutuma ni Rafiki yetu yeye ni mkubwa kuliko sisi, tukiuza mali tunagawana kinachopatikana, Elfu 50 hadi Laki 1, Wazazi wangu hawafahamu ninachokifanya, kilichonishawishi kufanya uhalifu ni marafiki, mapanga alikuja nayo Rafiki yangu yalikuwa kwenye mabegi"

Post a Comment

0 Comments