Mbowe "Mrema alikuwa ni mtu wa kuthubutu"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Moshi. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema aliyekuwa Mweneyekiti wa Chama Cha TLP, Augustine Mrema atakumbukwa kwa mengi katika nchi hii hasa katika harakati zake za kisiasa.

Amesema Mrema alikuwa ni kiongozi ambaye alikuwa akikosoa na kupinga pale panapostahili na kusukuma vita ya kutafuta haki, demokrasia, uhuru na maendeleo ya Watanzania kupitia vyama vya siasa.

Mbowe ameyasema hayo leo Alhamis 25, 2022 wakati akizungumza nyumbani kwa marehemu Mrema katika shughuli ya m,azishi ya mwanasiasa huyo katika Kijiji cha Kiraracha, Marangu, Mkoa wa Kilimanjaro.

"Mrema alikuwa naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani ya nchi katika nchi hii, pale alipoona kuna ulazima wa kukamilisha nafasi yake ili kuunga mkono juhudi za mageuzi katika Taifa alifanya hivyo," amesema


"Alikuwa ni kiongozi ambaye alikuwa na nafasi kubwa ya kufanya maamuzi magumu katika harakati za kisiasa ni hakika tutammiss katika harakati za kisiasa hapa nchini,"amesema Mbowe

Mbowe amesema, Mrema ni kilelezo bora cha watu wenye uthubutu, alionesha katika kipindi chote, aliweza kufanya uamuzi hata wengine walipoamini haiwezekani yeye alifanya."

Amesema, walifanya naye kazi katika nafasi mbalimbali, “nahata alipotaka kufanya maamuzi tofauti na matajio ya wengi alifanya hivyo. Mrema ameacha jina kubwa katika nchi hii, amegusa kila kona ya nchi yetu na sisi viongozi wa mageuzi tuliotembea nchi hii tumeona nyayo zao.”


Mbowe amemaliza kwa kumshuruku Mungu kwa maisha ya Mrema.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad