Mwigizaji Steve Nyerere Atoa Gari la Kusafirishia Mwili wa Mchekeshaji Erick Kisauti Baada ya Sintofahamu

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa


Mwili wa Mchekeshaji Erick Kisauti umeagwa jana Kibaha, Pwani na Wasanii na Wadau mbalimbali kabla na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Mwanza kwa ajili ya maziko.


Hapo awali kulikua na changamoto ya fedha iliyopelekea kuitisha michango ili mwili huo usafirishwe ambapo hata hivyo Mwigizaji Steve Nyerere @stevenyerere2 aliingilia kati na kujitolea gari la kuusafirisha mwili wa Mwigizaji huyo huku Wadau mbalimbali wakitoa michango mingine mbalimbali.


Mchekeshaji Sobogani Zablon maarufu Erick Kisauti alifariki alfajiri ya August 17 akiwa nyumbani kwa Ndugu zake Kibaha, Pwani na anatarajiwa kuzikwa Mwanza August 19.


_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad