Dear Parent..Siku Ukipata Nafasi ya Kukaa na Mwanao Mkumbushe HayaDear Parent

SIKU UKIPATA NAFASI YA KUKAA NA MWANAO MKUMBUSHE

1. Mkumbushe mwanao kuwa WIVU utamfanya amchukie Mtu ambaye alipaswa ajifunze kutoka kwake..

2. Mkumbushe Mwanao kuwa Msaada sio Haki yake asipopewa Asinung'unike atafute Chake...

3. Mkumbushe Mwanao kuwa Tumeona mazuri kwa watu waliokuwa wakiitwa wabaya na Tumeona mabaya kwa watu waliokuwa wakiitwa wazuri kwahiyo Aishi na kila mtu kwa akili...

4. Mkumbushe Mwanao kuwa bila Mungu hatofika popote.

5. Mkumbushe Mwanao kuwa Tunakosa Usingizi ili wanaotutegemea wapate kulala Vizuri...

6. Mkumbushe Mwanao kuwa Akiwa mzazi hata akiumwa hatotamani watoto wajue, maana tumaini lao pekee ni yeye...

7. Mkumbushe Mwanao kuwa Njia yake ikishanyooka Asithubutu kuwanyooshea vidole ambao Njia zao bado zina KONA...

8. Mkumbushe Mwanao kuwa Mtu atakae mpatia Bega la kuegemea wakati analia basi Asimsahau wakati amenyamaza...

9. Mkumbushe Mwanao kuwa anayemuona anacho kuna siku alikua hana kama yeye Msihi aendelee kutafuta...

10. Mkumbushe Mwanao kuwa akitanguliza kutafuta Umaarufu kabla ya Pesa basi ku-FAKE kutamtesa...

11. Mkumbushe mwanao kuwa Furaha ya kweli katika maisha ni pale tu anapokuwa na Amani ya Moyo bila kujali hali ya maisha aliyonayo...

12. Mkumbushe mwanao kuwa kuna maamuzi ili yamletee Faida lazima yamuumize kwanza...

13. Mkumbushe mwanao kwamba mlinzi anaemuona getini kwako, huku kwetu ni mlezi wa familia na ni mtu muhimu sana.

USIMDHARAU MTU MAISHA NI WATU, MAISHA NI KUTEGEMEANA.

*Zingatia Haya*

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

💥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad