Harmonize na Kajala Wafunga Ndoa Kidizaini Ndani ya Video ya Nitaubeba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Harmonize au Konde Boy; usiku wa kuamkia Septemba 23, 2022 Alhamisi ameachilia video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Nitaubeba ambao katika video yake, mchumba‘ke Kajala Masanja ndiye ameuza nyago kama video queen.

Harmonize au Harmo aliutoa wimbo huo jikoni wiki moja iliyopita ukiwa bila video (audio) na kuwashika wengi kwenye mitandao ya kijamii ambapo mapokezi yake yalikuwa ya aina yake kutokana na weledi wake aliouweka katika mashairi, lakini pia midundo ya aina yake.

Ujumbe mkubwa katika wimbo huo ni asilimia mia kwa mia amejitoa kwa mpenzi wake, Kajala na hilo pia kando na maneno linaweza likaonekana kwenye video kwa njia ya vitendo ambapo wengi walikuwa wanafanya mazoezi ya kungunga ndoa yao ambayo vyanzo vya ndani vinasema itakuwa hivi karibuni.

Harmonize na Kajala
kwenye video hiyo ambayo ndiyo inashika chati za juu kwa sasa mitandaoni, wanaashiria jinsi harusi yao itakavyokuwa, hasa ikizingatiwa kwamba baada ya kuvishana pete za uchumba miezi michache iliyopita, wengi wanasubiria harusi yenyewe kwa hamu.

Baada ya kuachilia video hiyo, Harmonize alikimbia kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuachia ujumbe maridhawa akidokeza kwamba huo ni mwanzo tu.

Harmonize anasema kuwa, video hiyo ni ‘dedication’ tosha kwa mpenzi wake, Kajala na aliifanya kwa njia ya kipekee kwa ajili yake –maneno ambayo ukisikiliza ngoma yenyewe utakubaliana nayo moja kwa moja bila kuhitaji uchambuzi wa kina.

“Nilifanya hii kwa ajili ya mtu nimpendaye. Ni wakati wako sasa pia kumuimbia unayempenda. Hebu tafakari jinsi hiyo siku yetu itakavyokuwa, siku yetu muhimu. Ahsante sana meneja wangu mkubwa, mke wangu, Fridah Kajala kwa kusababisha hili litokee,” Harmonize anamsifia Kajala.

Pia Harmonize anafunguka kuwa kila neno na kila tukio katika wimbo huo pamoja na video yake ni ishara tu ya kila kitakachotokea katika siku ya ndovu kumla mwanawe, siku ya kufunga pingu za maisha ambayo wangali bado kuiweka wazi.

“Jua kwamba kila neno kama siyo herufi katika wimbo huu linaelezea kiasi gani mimi nakupenda. Inshallah Mungu atuongoze pamoja na wapendanao wote. Tufike hiyo siku,” Harmonize alimalizia.

Kwa upande wake Kajala amemjibu; “Unajua una maana gani kwenye maisha yangu sina aja kuongea mengi jua nakupenda sana Mungu akuweke kwa ajili yangu na mapacha…”

Stori; Khadija Bakari, Dar

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad