Hizi Hapa Sababu za Glazers Kuamua Kutoiuza Manchester United…

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Thamani ya Manchester United kwenye Soko la Hisa la New York ilishuka kwa zaidi ya pauni milioni 500 kufuatia ripoti kwamba Glazers wameamua kutoiuza.

Miezi tisa iliyopita wamiliki walitangaza mauzo kamili kuwa miongoni mwa chaguzi zinazozingatiwa kama sehemu ya ukaguzi wa kimkakati katika kilabu cha Old Trafford.

Sheikh Jassim na Sir Jim Ratcliffe walitoa ofa za kutaka kuinunua United, lakini mchakato wa kuichukua unaendelea kusuasua huku mashabiki wakiachwa gizani wakiandamana dhidi ya Glazers.

Matumaini ya mauzo kamili yalionekana kupotea wakati Mail on Sunday iliripoti kwamba wamiliki wanaiondoa klabu sokoni na watajaribu kuiuza tena 2025.

Ripoti hiyo ilisababisha zaidi ya pauni milioni 500 kuondolewa kwenye bei ya hisa ya United siku ya Jumanne.

Mtaji wa soko wa United – thamani ya kampuni kwenye soko la hisa – ulisalia kwa $3.15bilioni (£2.5bilioni) baada ya kushuka kwa asilimia 18.22.

Mapema mwaka huu familia ya Glazer iliripotiwa kuwa na thamani ya United kwa £6bn.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad