Ahmed Ally: Simba tuna mengi ya kujifunza kwa Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ahmed Ally: Simba tuna mengi ya kujifunza kwa Yanga


Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amewapongeza wapinzani wao, Yanga SC kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa mara ya 30 sasa huku wakiwa wamechukua ubingwa huo mara tatu mfululizo.


Ahmed amesema hayo baada ya Yanga kutwaa Ubingwa huo jana kwa kumfunga Mtibwa Sugar na kufikisha alama 71 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.


“Kwenye maisha unapopata kitu kibaya kinakuongezea nguvu ya kutafuta sare ambayo tumeipata dhidi ya Kagera Sugar imetuongezea nguvu ya kupambana kupata nafasi ya pili. Vita yetu rasmi ni kuhakikisha tunaipata nafasi ya pili ili twende tukashiriki ligi ya mabingwa msimu ujao.


“Tunawapongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa, haikuwa safari nyepesi, mbio zilikuwa kubwa lakini lazima mtu mmoja awe bingwa. Hatuna budi kumpongeza yanga kwa kutwaa Ubingwa.


“Sisi kama Simba tuna mengi ya kujilaumu, tuna mengi ya kujifunga, kujikosoa na kujirekebisha. Tunao wajibu wa kukaa chini na kufikiria tunakosea wapi msimu wa tatu sasa bila taji.


“Hii imemalizika, sasa tunapigania nafasi ya thamani ya ushindi wa pili. Kwa sasa tunalingana alama na Azam, lazima tuhakikishe tunapata nafasi ya pili,” amesema Ahmed.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini: 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad