Ishu ya Simba na Mayele, Show Nzima Iko Hivi..Try Again Atoa Matumaini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ishu ya Simba na Mayele, Show Nzima Iko Hivi..Try Again Atoa Matumaini


Uongozi wa Simba rasmi umeingia katika rada za kumtaka kumsajili mshambuliaji wa Pyramids FC ya nchini Misri, Fiston Mayele.

Simba imepanga kukifanyia maboresho makubwa kikosi chao, ili kifanye vema katika msimu ujao.

Mayele aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, ni kati ya wachezaji waliokuwepo katika mipango ya Simba katika msimu ujao.

“Tunaangalia uwezekano wa kumpata Fiston Mayele kwa mkopo kutoka Pyramids FC, tumeshatuma maombi Egypt.” Salim Abdallha ‘Try Again’ – Mwenyekiti wa Bodi ya Simba.

Hivi karibuni Simba walipokuwa Misri kwenye mchezo wa marudio dhidi ya Al Ahly, Mayele aliitembelea timu hiyo ambapo alipata nafasi ya kuongea na aliyekuwa kocha wa Simba, Benchikha pamoja na viongozi.

Alipohojiwa kuhusu kuitembelea timu hiyo wakati wanajindaa na mechi kali ya kutafuta mshindi wa kwenda Nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Mayele alisema kuwa ameenda kuonyesha upendo na kuwapa hamasa wachezaji.

Simba hivi sasa inapitia kipindi kigumu kwenye kikosi chache haswa eneo la ushambuliaji, ambapo mara kadhaa washambuliaji wao wamekuwa wakikosa nafasi za wazi za kufunga magoli.

Taarifa kutoka Simba zinadai kuwa pamoja na kwamba kutafanyika mchujo mkubwa wa wachezaji kutemwa, ila jina la Mayele lilipewa baraka ya kusajiliwa ndani ya kikosi hiko na Banchikha.

Endapo dili hili litafanikiwa , inamaana Mayele ambaye hivi sasa amepooza kulingana na alivyokuwa Yanga, atakuwa anarudi kucheza Ligi ya NBC kwa mara ya  pili.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini: 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad