Mrema Atangaza Kumuunga Mkono Mgombea Urais wa CCM John Magufuli Wakati Chama Chake TLP Kina Mgombea Urais Pia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Leo katika mkutano wa CCM katika jimbo la vunjo, akihutubia nyomi ya watu, mgombea urais wa CCM John Pombe Magufuli alimwombea kura mgombea wa TLP, Augustino Mrema kwa wakazi wa Vunjo kwamba wamchague kuwa mbunge wao huku mgombea wa CCM wa jimbo hilo Innocent Shirima akiwa pembeni yake akishangaa bila kuamini.

Magufuli alisema pia kwamba mrema akichaguliwa atamwingiza kwenye baraza lake ya mawaziri.

Wakati hayo yakijiri viwanja vya himo, Mrema alikuwa njia panda na wakati Magufuli amemaliza mkutano wake alipita na 'entourage' yake kuelekea Same.

Mrema alikuwa amesimama anaongea na watu hapo njia panda, msafara wa Magufuli ulimpita Mrema kuelekea Same, lakini baada ya dakika 10 convoy ya Magufuli ilirudi njia panda ili kumsalimia mrema, wakazi wa Vunjo walifurika na Magufuli alimwomba Mrema aongee kidogo. Mrema alimsifia Magufuli kwa barabara alizojenga katika jimbo la Vunjo.

Magufuli nae alirudia akisema mbatia hafai kuwa mbunge ila wamchague Mrema ambaye ni jembe na mchapakazi kama yeye na watu walilipuka kwa shagwe.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Replies
    1. EEH,HATA KAMA NI MWEHU KASIKILIZWA NA KUELEWEKA NA NDIO MAANA WATU WAKALIPUKA KWA SHANGWE,MWEZI MCHANGA.

      Delete
  2. tenaa cyo mwehu kiidogo!! mkubwa tu!! sasa yeye mwenyekiti, na chama chake kinamgombea, halafu anawashauri wanachama wake ambao cyo wengi wamuunge mkono mtu mwingine! mzima kweli huyu!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. HUYU NI MTU WA KAZI,ATACHAGUA MTU ASIYEMCHAPA KAZI?KISA NI WA CHAMA CHAKE?KACHUNGUZA KAAMBIWA HAMFAI KWENYE UONGOZI WAKE NA KUMBE MREMA KAFANYA KAZI NZURI,HACHAGUI BINAMU WALA RAFIKI,KAMA WEWE NI MVIVU HUNA MAADLI ATAANZA NA WEWE

      Delete
  3. MAGUFULI AWATAKA MWANACHI WA VUNJO KUMPA KURA MREMA WA TLP KWA MAENDELEO YAO NA CIO MGOMBEA WA CHAMA CHAKE CHA CCM,KWELI POLENI CCM HUYU NI MGOMBEA BINAFI ALEE VAAA KOTI LA CCM LENYE CHAWA WEEEEEENGI AKIPATA LAZIMA ATALIVUA,SASA TUSIFIKE HUKO NJIA RAHISI TWENDE NA UKAWA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mafisadi,wavivu hawana na nafasi kwa Magufuli,kwa nini kwingine kote awadi wagombea ubunge wa CCM hapo asifanye hivyo?kuna walakini kwa mgombea wa CCM,kama yupo aliyefanya kazi vizuri apite hata kama ni chama pinzani.
      BADO MTAMJUA MAGUFULI VIZURI AKIWA RAIS,chagua Magufuli.Mtu wa kazi.

      Delete
  4. Toba kachoka mwili hadi akili
    Nashangaa Mtu mzima ovyo hata hajui kampeni ampigie Nani
    Makongoro tazama wagonjwa hawa

    ReplyDelete
  5. YAANI MWAKA HUU NI VITUKO BILA KUSAHAU MGUFULI NAE KAACHA CHAMA CHAKE CHA CCM ET AKIMPIGIA DEBE MGOMBEA WA TLP, HUU NI UCHAGUZI WA KIHISTORIA WATU FULL KUCHANGANYIKIWA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. NGUVU ya UKAWA hiyo, inawafanya wachanganyikiwe!! peopleezzzzzzzzzzzzzzzz!!! powerrrrrrrrr!!!!!

      Delete
  6. LOWASSA NYWELE NYEUPE,MOYO MWEUPE,NJIA YA IKULU NYEUPEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

    ReplyDelete

Top Post Ad