Amanda Abanwa Kuhusu Ukimwi, Afunguka

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Amanda Poshi amefungukia taarifa zinazomhusisha yeye kuugua maradhi ya Ukimwi.

Amanda amefunguka hayo baada ya kuvuja kwa picha zake zinazomuonesha akiwa amepungua mwili na kusababisha gumzo litawale kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii watu wakihusisha kukonda kwake na ugonjwa huo ndipo mwanahabari wetu alipombana, akafunguka:

“Nina desturi ya kupima kila wakati, hawanipi presha. Nimeshapima mwaka 2013 kibao na mara ya mwisho ni mwaka jana lakini hayo madai yamekuwa yakiibuka mara kwa mara wananiboa kweli mbaya zaidi hao wanaolazimisha nipime wao wenyewe hawapimi.
amanda

“Nilipokuwa mnene presha ilikuwa inashuka kila mara, namshukuru Mungu kwa sasa nimeanza gym niko imara, nimepungua mwili vizuri.”

baada ya kusema hayo Amanda alimtumia mwanahabari wetu vyeti vyake mbalimbali vyenye majibu ya Ukimwi vikionesha yupo safi.
_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kuonyesha vyeti vya kuwa huko mzima haimanishi kuwa huko mzima!! Vyeti vingi vya bongo ni majanga matupu!! Ila nakuombe afya njema, muda ukifika yote yataonekana.

    ReplyDelete
  2. na wewe unayemnyooshea mwenzio kidole angalia unaweza tangulia ukamuacha! wote tupo duniani bado. chunga sana kauli yako!

    ReplyDelete
  3. Amanda yuko safii,

    ReplyDelete

Top Post Ad